Majmaa ya Shekhe Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya inaendelea kugawa futari kwa mazuwaru ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Msaidizi wa kiongozi wa Majmaa, Muhandisi Ahmadi Haamid Sarhani amesema “Majmaa Shekhe Kuleini inaendelea kupokea mazuwaru wanaokwenda katika mji wa Karbala ndani ya mwezi wa Ramadhani na kuwapa huduma bora zaidi siku zote za mwezi huu mtukufu”.
Akaongeza kuwa “Majmaa inagawa zaidi ya Sahani (500) za chakula kila siku tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhani”.
Majmaa inapokea mazuwaru kutoka mikoa tofauti na nchi tofauti pamoja na wageni wanaoletwa na Ataba tukufu.