Katika hospitali ya Alkafeel.. katibiwa mgonjwa mwenye tatizo la saratani inayo sambaa.

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kumtibu mgonjwa mwenye tatizo la saratani inayo sambaa iliyompelekea kudhofika afya yake.

Daktari bingwa wa upasuaji Dokta Ali Almayali amesema “Tumefanya upasuaji wenye mafanikio kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka minne aliyekua na tatizo la saratani inayosambaa kwenye utumbo mnene”, akabainisha kuwa “Tumetumia vifaa-tiba maalum vilivyo ingizwa hapa Iraq hivi karibuni, vifaa hivyo vinapatikana maeneo machache duniani, vinatumia kemia-joto”.

Akaongeza kuwa “Baada ya kufanya vipimo na kubaini tatizo tuliamua kumfanyia upasuaji wa kisasa kwa ajili ya kuondoa saratani”, akasisitiza kuwa “Mgonjwa anaendelea vizuri baada ya upasuaji na ataruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kukamilika matibabu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: