Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imeendesha mashindano ya (kisa cha aya) kwa waliohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu awamu ya nne.
Kiongozi wa Habari katika Maahadi Dokta Israa Akarawi amesema “Shindano la kisa cha aya awamu ya nne, ni shindano maalum kwa waliohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu chote katika mkoa wa Najafu ndani ya mwezi wa Ramadhani, washiriki walikua (20)”.
Akaongeza kuwa “Kamati ya majaji imeundwa na walimu wa Maahadi, wameandaa maswali kwa ufundi mkubwa na kuzingatia maana za maneno”.
Kuhusu namna ya shindano amesema “Kamati ya majaji inasoma swali linalotaja kisa ndani ya Qur’ani, na haafidh anatakiwa kukumbuka kisa na kusoma aya zinazohusiana na kisa hicho”.
Shindano hili linaonyesha umuhimu wa kufahamu visa vya Qur’ani tukufu, hususan kwa mtu aliyehifadhi Qur’ani, anatakiwa aelewe maana, madhumuni na visa vya Qur’ani, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa habari katika Maahadi.