Idara ya Fatuma binti Asadi na idara zingine zilizo chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake katika Ataba tukufu, zimehitimisha ratiba ya usomaji wa Qur’ani kwa wanawake ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara imehitimisha vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa wanawake katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), kikao cha ufungaji wa ratiba hiyo kimefanywa ndani ya ukumbi wa mikutano”.
Akasema kuwa “Hafla imehusisha usomaji wa Dua, muhadhara kuhusu kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuandika barua kwa Imamu Hujjat (a.f), kufanya mashindano katika hadithi za Ahlulbait (a.s), ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi waliohifadhi hadithi na wasomaji wa Qur’ani walioshiriki”.
Akaongeza kuwa “Lengo la ratiba ya mwezi wa Ramadhani, kuimarisha mafungamano na kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi huu mtukufu kwa wanawake sambamba na kufundisha masomo ya Fiqhi, Qur’ani na Sira”.