Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa mihadhara kuhusu Zakatul-Fitri katika msikiti wa Imamu Hussein (a.s) uliopo Mombasa nchini Kenya.
Mihadhara imetolewa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya muwakilishi wake Shekhe Jamali Kasole.
Muhadhara umejikita katika kufafanua umuhimu wa Zakatul-Fitri sambamba na kusherehesha vipengele vinavyofungamana na zaka hiyo.
Wahudhuriaji wakapewa nafasi ya kuuliza maswali na kupata majibu kutoka kwa Shekhe Kasole.
Ratiba hiyo inasaidia kujenga uwelewa na mshikamano katika jamii ya watu wa Mombasa, sambamba na kuwashajihisha kutoa Zaka na kufanya mambo mema wakati huu wa mwezi wa Ramadhani.