Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kinaendesha vikao darasa katika mwezi wa Ramadhani kwa wanawake wa Baghdad.
Mkuu wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Kituo kimefanya kikao darasa kilicho husisha wanawake kutoka Baghdad, wametembelea husseiniyya na Abulfadhil Abbasi (a.s) na kushiriki katika taasisi ya Haamilul-Juud ya Karbala katika kuhuisha nyusiku za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Akaongeza kuwa “Ratiba imehusisha muhadhara wenye anuani isemayo (Mwanaadamu anahadhi kubwa) uliotolewa na (Sundusi Muhammad), ameeleza umuhimu wa kutakasa nafsi ili kupata ukamilifu na furaha, ikafuatiwa na mashindano mbalimbali yaliyosimamiwa na bibi (Ikhlasu Jawaad)”.
Harakati hiyo kwa mujibu wa Alhafaar, inawajenga wanawake kifamilia, kinafsi na kidini, inasaidia kulinda utulivu wa familia na kujenga kizazi kinachotambua majukumu yake na kinachoweza kupambana na changamoto za Maisha kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).