Atabatu Abbasiyya imefuturisha wastafu wake.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefuturisha waliokuwa wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussawi amesema “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, umealika wastafu wake kuja kufuturu, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi zao wakati walipokuwa wakihudumia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Jambo hili ni ujumbe wa wazi kwa watumishi, siku za kutoa huduma kwa mwezi wa familia huisha haraka, mara mtu hujikuta kafikisha umri wa kustafu, jambo hili linatusukuma wote kutumia vizuri muda tuliobahatika kuhudumia mazuwaru Jirani na malalo takatifu”.

Wastafu wamefurahi sana kwa heshima waliyopewa na kubakizwa majina yao katika orodha ya wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kuwapa mualiko huu wa futari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: