Maukibu ipo Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mkabala na mlango wa Qibla, inaendelea na huduma ya kugawa chai kwa mazuwaru baada ya futari sambamba na kugawa vyakula vyepesi.
Maukibu huanza kutoa huduma wakati wa futari hadi wakati wa daku, nayo ni sehemu ya huduma wanazopewa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya idara ya Masayyid katika Ataba tukufu.
Atabatu Abbasiyya inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wanaokuja Karbala, sehemu ya huduma hizo zinatolea katika Majmaa ya Shekhe Kuleini na sehemu zingine katika kipindi chote cha mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.