Atabatu Abbasiyya tukufu imefuturisha watu wa mawakibu Husseiniyya katika mji wa Karbala na viunga vyake.
Futari hiyo imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Yasiri amesema “Kwa ajili ya kudumisha mawasiliano na wahudumu wa Imamu Hussein (a.s) kutoka katika mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika mji wa Karbala na viunga vyake, tumeandaa futari kwa ajili yao kama sehemu ya kupongeza kazi wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Futari imeandaliwa katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na watu wengi miongoni mwa wajumbe wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka maeneo tofauti ya mji wa Karbala, akasema kuwa Atabatu Abbasiyya imekua ikiimarisha ushirikiano na wahudumu wa Imamu Hussein (a.s) kutokana na huduma wanazotoa kwa mazuwaru wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.