Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya anapokea wanaokuja kutoa pongezi za Idul-Fitri.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, anapokea watu wanaokuja kutoa pongezi za Idul-Fitri.

Katika kikao cha kupokea wageni hao amehudhuria pia katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, wamepeana pongezi na kutakiana kheri na baraka za sikukuu.

Ataba imepokea viongozi wa mkoa wa Karbala na raia wa kawaida, waliokuja kutoa pongezi za Idul-Fitri katika mazingira yaliyojaa amani na furaha.

Hali kadhalika wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wameingia kutoa pongezi ya sikukuu na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu arejeshe tukio hili huku wananchi wakiwa katika utulivu na amani.

Sayyid Swafi amemuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada za watu wote, ailinde Iraq na raia wake, aineemeshe kwa utulivu na amani, akawashukuru wote waliokuja kutoa pongezi za sikukuu na akawatakia kheri na amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: