Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Alkafeel kimetembelea Darul-Furqaan (kituo cha kulelea mayatima) kwa lengo la kuimarisha mawasiliano na jamii.
Ziara hiyo imeshirikisha walimu kadhaa chini ya utaratibu wa kuonyesha kujali misingi ya uislamu, jamii na umuhimu wa kulea mayatima na mafukara katika uislamu.
Ziara imehusisha utoaji wa zawadi kwa mayatima na mafukara waliopo kituoni, ikiwa kama sehemu ya kufanyia kazi hadithi tukufu ya Mtume inayohimiza kulea mayatima na kujenga mapenzi na mshikamano katika jamii.