Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, kimeendesha swala ya Idul-Fitri katika nchi ya Kenya.
Mmoja wa viongozi wa idara ya Tablighi katika Markazi Sayyid Muslim Aljaabiri amesema “Markazi imeendesha swala ya Idul-Fitri kwenye msikiti wa Imamu Hussein (a.s) katika kaunti ya Kwale jijini Mombasa nchini Kenya”.
Akaongeza kuwa “Muwakilishi wa Markazi Shekhe Jamali Abdallah Kasole amewaswalisha waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) swala wa Idul-Fitri”.
Swala ya Idi ni moja ya utamaduni wa Dini ambao huchangia kujenga mapenzi, amani, umoja na mshikamano katika jamii, kwa mujibu wa maelezo ya Aljaabiri