Atabatu Abbasiyya imepokea idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya pili ya Idul-Fitri.
Atabatu Abbasiyya imetumia uwezo wake wote kurahisisha harakati za mazuwaru waliokuja kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, sambamba na waliokuja kutoka nchi tofauti za kiarabu na kiislamu.
Mazingira ya Ataba yamejaa muonekano wa furaha, uliojaa mazingira ya kiibada katika haram takatifu.