Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya imepokea mamia ya mazuwaru waliokuja kuangalia mali-kale zake.
Sayyid Ali Husseini kutoka idara ya Habari amesema “Ukumbi wa makumbusho ya Alkafeel umepokea mazuwaru wengi waliokuja kutembelea mji wa Karbala na malalo ya mwezi wa bani Hashim (a.s) katika siku za Idul-Fitri”.
Akaongeza kuwa, ukumbi wa makumbusho unapokea mazuwaru kuanzia asubuhi hadi usiku, kwa lengo la kutoa nafasi kubwa zaidi ya kuangalia mali-kale za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).