Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya nadwa kwa kundi la vijana wa mji mkuu wa Baghdad.
Nadwa hiyo imesimamiwa na kituo cha kitamaduni Multaqal-Qamaru, nayo ni miongoni mwa ratiba za kitamaduni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Nadwa ilikuwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Umuhimu wa kutambua misingi ya sheria) iliyowasilishwa na Shekhe Harithi Dahi, amefafanua kwa kina kuhusu misingi ya sheria katika uislamu na umuhimu wa kuzitambua, ukajadiliwa utata wa kifikra ambao huibuliwa kuhusu mada hiyo.
Harakati hii ni sehemu ya ratiba ya kituo cha kitamaduni Multaqal-Qamaru kinacho lenga kuhudumia vijana na kuwapa malezi sahihi kielimu, kitamaduni na kujenga uzalendo.