Mradi wa ukanda wa kijani umepokea mamia ya familia katika siku za Idul-Fitri.

Mradi wa ukanda wa kijani chini ya Atabatu Abbasiyya, umepokea mamia ya familia katika siku za Idul-Fitri.

Na bado unaendelea kupokea familia za mazuwaru katika siku hizi za Idul-Fitri.

Ataba tukufu imetengeneza sehemu ya mapumziko kwa familia za watu wa Karbala na mazuwaru, kwa kufanya mradi wa ukanda wa kijani wenye mandhari nzuri ya kupendeza, sambamba na kuweka mahitaji yote ya lazima kwa mapumziko ya familia.

Mradi huo unasehemu (24) za kupokelea wageni, kila sehemu ina vyoo, sehemu za kupumzika, sehemu za michezo ya watoto, sehemu za ufugaji wa Samaki, sehemu ya kubanika nyama na Samaki, sehemu za maporomoko ya maji, sehemu zote zimepambwa na bustani nzuri za kupendeza.

Familia zilizo tembelea ukanda wa kijani kibichi zimesema kuwa, hakika Ataba tukufu imetengeneza sehemu nzuri sana kwa mapumziko ya familia za watu wa Karbala, hii ni sehemu tulivu isiyokuwa na fujo kama zilizopo mjini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: