Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kutibu kijana mwenye umri wa miaka ishirini kutoka mkoa wa Basra aliyekuwa na tatizo la kuziba mirija ya ubongo, kwa kutumia upasuaji wa kisasa (Naadhuurah).
Daktari bingwa wa upasuaji Dokta Yahaya Abdurazaaq Aljahishi amesema “Mgonjwa anatoka mkoa wa Basra, alikua na maumivu makali ya kichwa na kutapika mara kwa mara, alifanyiwa vipimo vya kina kutambua sababu ya ugonjwa wake”.
Akaongeza kuwa, “Vipimo vikaonyesha kunatatizo kwenye ubongo wake kutokana na kuziba kwa mrija wa ubongo kulikopelekea ukavu katika sehemu ya ubongo”.
Akafafanua kuwa “Ndipo tulipoamua kumfanyia upasuaji wa kisasa kwa kutumia Naadhuri badala ya upasuaji uliokuwa unafanywa zamani, kutokana na vifaa vya kisasa vilivyopa katika chumba cha upasuaji na umahiri wa madaktari tumefanikiwa kufanya upasuaji wenye tija na mgonjwa ameondoka hospitalini baada ya upasuaji akiwa na afya nzuri”.