Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza majina ya washindi wa shindano la kijana wa Alkafeel lililofanywa kwa njia ya mtandao.
Imepigwa kura ya kutafuta washindi katika majibu (200) sahihi kutoka katika zaidi ya majibu (3500) yaliyotufikia, ambapo wamechaguliwa washindi thelathini kati yao.
Kitengo kimeandaa zawadi za pesa na tabaruku kwa washindi, zawadi hizo zimetolewa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mashindano ya mwezi wa Ramadhani ni moja ya harakati ambayo hufanywa na kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu.