Maktaba ya Ummul-Banina ya wanawake imechapisha toleo la (205) la jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s).

Hivi karibuni Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) katika Atabatu Abbasiyya imechapisha toleo la (205) la jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s) ambalo hutoka kila mwezi.

Jarida hilo ni chapisho maalum linaloandika maswala ya wanawake kutoka katika Ataba tukufu za Iraq kuanzia mwaka (2003).

Chapisho jipya linavipengele vya Fiqhi, Aqida, Qur’ani, Malezi, Elimu, Utamaduni, Jamii, Afya pamoja na mambo mengine.

Mada hizo zimeandikwa kwa anuani tofauti, miongoni mwake ni: (Kwa ajili ya kudhihiri, Wanashindana katika kheri, Wakinamama, Undani wa roho, Dini bora kupendana kwa ajili ya Allah, Rehema iliyosambaa).

Mnaweza kusoma jarida hilo kupitia toghuti ya jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: