Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya harakati tofauti za kidini katika nchi ya Tanzania barani Afrika.
Mmoja wa watumishi wa idara ya Tablighi katika Markazi Dirasaati Afriqiyya Sayyid Muslim Aljaabiri amesema “Mwaka huu Markazi imeandaa ratiba maalum katika bara la Afrika, iliyojumuisha vipengele vya kidini, kitamaduni na kielimu”.
Akasema kuwa “Ratiba imehusisha swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ghadiir uliopo (Kigogo) jijini Dar es salaam nchini Tanzania, iliyohudhuriwa na waumini wengi miongoni mwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Khatibu wa Ijumaa Shekhe Jamali Abdallah Kasole amesema kuwa “Khutuba ya Ijumaa ilijikita katika kubainisha utukufu wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na baadhi ya tabia njema anazotakiwa kupambika nazo kila mtu maishani mwake”.
Markazi Dirasaati Afriqiyya kupitia ratiba zake inalenga kufundisha masomo ya Fiqhi na Aqida sahihi ya uislamu halisi, sambamba na kujenga uwelewa wa kitamaduni na kijamii.