Atabatu Abbasiyya imetoa mualiko kwa chuo kikuu cha Basra.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetoa mualiko kwa chuo kikuu cha Basra, kichague wanafunzi wake watakaoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu imepewa jina la (Juu ya muongozo wa mwezi) awamu ya nne, chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji unastawi) katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ushiriki wa wanafunzi (4500) takriban, kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.

Rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ali Azhar amesema (Kamati inayoratibu mahafali imetoa mualiko rasmi kwa chuo kikuu cha Basra, kichague wanafunzi wake watakaoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq itakayo fanywa tarehe kumi na tisa mwezi wa nne”.

Akaongeza kuwa “Utoaji wa mialiko ni sehemu ya mkakati wa maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq itakayokuwa na vipengele tofauti”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya mahafali kubwa za wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq kutoka mikoa tofauti, na kuwafanya wahitimishe safari yao ya elimu ndani ya malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: