Mahafali ya wahitimu imepewa jina la (Juu ya muongozo wa mwezi) awamu ya nne chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji umestawi), mahafali hiyo ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, washiriki ni (4500) kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.
Imepandwa miti na mauwa ya mapambo katika eneo la nyumba za Abulfadhil Abbasi (a.s), zilizopo Barabara ya (Najafu – Karbala), ambapo ndio kituo kukuu cha kupokea wanafunzi.
Miti na mauwa yamepandwa kwa mpangilio mzuri unaoendana na mahafali itakayofanywa, ukizingatia kuwa miche yote imeandaliwa na sisi wenyewe.
Atabatu Abbasiyya tukufu inatarajia kufanya mahafali kubwa ya wahitimu wa vyuo vikuu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, ambao wanakuja kuhitimisha safari yao ya masomo mbele ya malalo takatifu.