Chuo kikuu cha Alkafee kimefanya kumbukizi ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya majlisi ya kumbukumbu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Majlisi imesimamiwa na kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi (saikolojia) katika chuo, imehudhuriwa na walimu, wanafunzi na watumishi wa chuo.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Mahadi Falandar kutoka Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ukafuata muhadhara uliotolewa na Sayyid Jafari Murawiji, ameongue kuhusu umuhimu wa kulinda misikiti na maeneo matakatifu ya Mitume na waja wema, na kurudi katika utamaduni wa kiislamu unaofundishwa na Qur’ani tukufu, sambamba na kuishi kwa misingi ya kuheshimiana na kusaidiana katika jamii.

Akasisitiza umuhimu wa kupambana na vitendo vya ukatili na ubaguzi vinavyo lenga maeneo matakatifu kwa waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: