Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imesema: Tumehitimisha Qur’ani zaidi ya mara (3000) wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa, tumehitimisha Qur’ani zaidi ya mara (3000) ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imekhitimu Qur’ani zaidi ya mara (3000) ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa Maahadi wamefanya kazi kubwa ndani ya mwezi wa Ramadhani, wamesimamia vikao vingi vya usomaji wa Qur’ani kwa lengo la kunufaika na utukufu wa mwezi huo”.

Akabainisha kuwa “Vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa njia ya moja kwa moja na njia ya mtandao vimefanywa katika ofisi za Maahadi, matawi yake, misikiti na huseiniyya za ndani na nje ya Iraq, wanawake wameshiriki kwa wingi katika ratiba hiyo”.

Idara ya Qur’ani katika vyuo imeshuhudia ushiriki mkubwa wa wanafunzi mwaka huu, vilifanywa vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa njia ya uhudhuriaji na mtandao kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi za Iraq waishio hosteli (bwenini).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: