Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimeboresha upya App yake ya (Maarifa ya turathi) na kurahisisha matumizi yake.
Katika muonekano mpywa wa sasa App inamilango saba, ambayo ni (Habari za maarifa, Maktaba ya maarifa, Wanachuoni wetu, Mashindano, Picha za maarifa na vipande vya video).
App inahusu turathi za kiislamu, inamamia ya maudhui, Makala, machapisho, Habari, picha za turathi. Mlango wa mashindano utatoa nafasi ya kuongeza maarifa kwa watumiaji wa App sambamba na utoaji wa zawadi mbalimbali.
Unaweza kupakua App hiyo kupitia Play Store katika simu zenu za mkononi, kwa jina la (Maarifa ya turathi).