Rais wa kamati ya malezi na elimu anapokea wanafunzi wanaokuja kushiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu.

Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu na wajumbe wa idara yake, Dokta Abbasi Rashidi Didah Mussawi, anapokea wanafunzi wanaokuja kushiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq awamu ya nne.

Mahafali ya wahitimu imepewa jina la (Juu ya uongofu wa mwezi) awamu ya nne chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji umestawi) ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, washiriki ni wanafunzi (4500) kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.

Misafara ya wahitimu wa vyuo vikuu imewasiri katika nyumba za Abulfadhil Abbasi (a.s) sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya makazi yao, siku ya Alkhamisi, mahafali itaanza kesho siku ya Ijumaa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s),

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq tarehe kumi na tisa mwezi wa nne, yenye vipengele tofauti vinavyo lenga kuwajenga wahitimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: