Kukamilika ratiba ya asubuhi katika mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya asubuhi katika mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq awamu ya nne.

Ratiba ya asubuhi imehusisha utoaji wa kiapo cha kuhitimu, kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na kufanya matembezi katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Mahafali inalenga kuwapongeza wahitimu wa vyuo kuanzia kaskazini hadi magharibi mwa Iraq, umekua utamaduni wa Atabatu Abbasiyya kufanya mahafali hiyo.

Mahafali ya wahitimu imepewa jina la (Juu ya uongofu wa mwezi) awamu ya nne chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji umestawi) ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, washiriki ni wanafunzi (4500) kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.

Mahafali hiyo ni tukio muhimu ambalo hufanywa na Atabatu Abbasiyya, huwa na vipengele tofauti vinavyo lenga kuwajenga wahitimu na kuhakikisha Maisha yao ya baada ya masomo yanaanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: