Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unatoa huduma ya chakula kwa washiriki wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umetoa huduma ya chakula kwa washiriki wa mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.

Rais wa kitengo cha mgahawa Sayyid Aadil Hamami amesema “Wahudumu wa mgahawa wanagawa chakula mara tatu kila siku kwa wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq wanaoshiriki kwenye mahafali inayosimamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi ya mahafali hiyo yalianza mapema na yamefanywa kwa kiwango cha juu katika ndazi zote”.

Mahafali ya wahitimu imepewa jina la (Juu ya uongofu wa mwezi) awamu ya nne chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji umestawi) ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, washiriki ni wanafunzi (4500) kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: