Atabatu Abbasiyya imezawadia marais wa vyuo vikuu vinavyoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo.

Atabatu Abbasiyya tukufu imezawadia marais wa vyuo vikuu vinavyoshiriki kwenye mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq awamu ya nne.

Mahafali ya wahitimu imefanywa kwa jina la (Juu ya uongofu wa mwezi) chini ya kaulimbiu isemayo (Kutoka ardhi ya Karbala utoaji unastawi), kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kwa ushiriki wa wanafunzi (4500) kutoka vyuo (54) vya serikali na binafsi.

Waliosimamia shughuli ya utoaji wa zawadi ni kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, makamo katibu mkuu Sayyid Abbasi Mussawi, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Ataba, ambao ni Abbasi Dida Mussawi, Dokta Muhammad Ashiqar, Sayyid Jawadi Hasanawi, Sayyid Kadhim Abadah na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nurus Dahani, ikiwa kama sehemu ya kuthamini ushiriki mkubwa wa vyuo kwenye mahafali hiyo.

Mahafali imeanza asubuhi ya Ijumaa, ikiwa na wanachuo zaidi ya (4500), baadhi ya viongozi wa kitaifa, wazazi na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mahafali imelenga kuonyesha picha halisi ya matokeo ya vyuo vikuu vya Iraq kwa wananchi, imealika wanachuo kutoka Dini na jamii tofauti, kwa Pamoja wamesoma kiapo cha kuhitimu masomo yao na utii kwa taifa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: