Hafla inasimamiwa na shule za Al-Ameed za wavulana chini ya kitengo, itaanza tarehe 21 April 2024m.
Rais wa kamati ya maandalizi Sayyid Muthanna Daaimi amesema “Kitengo cha malezi na elimu kinasimamia hafla ya vijana wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria, kwa lengo la kuwajengea misingi ya kuwajibika”.
Akaongeza kuwa “Maandalizi yanaendelea vizuri sambamba na kuandaa ratiba maalum ya hafla hiyo”.
Akasema kuwa “Idadi ya wanafunzi watakaoshiriki kwenye hafla hiyo ni zaidi ya (460)”.
Kitengo cha malezi na elimu kimetaja ratiba ya hafla ya vijana wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria itakayofanywa ndani ya majengo ya shule za Al-Ameed.