Idara ya wahadhiri tawi la wanawake imetengeneza vitambulisho vya mabinti wanaoshiriki kwenye hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha kazi ya kuandaa vitambulisho vya washiriki wa hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa wanafunzi wa shule za mkoa wa Karbala na Qadisiyya, kupitia mradi wa (Maua ya Fatwimiyyah) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu), hafla inafanywa kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Karbala, itakuwa na washiriki (4500) kutoka shule (89).

Wahudumu wa Idara wamekamilisha utengenezaji wa vitambulisho maalum vya washiriki wa hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria, vitambulisho vimeandikwa taarifa binafsi za mshiriki, picha, majina matatu na jina la shule anayosoma.

Hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria inawajenga kidini na kitamaduni, kwani hufundishwa udhu, swala, usomaji wa surat Faat-hah sambamba na kuwajenga waweze kuhimili majukumu ya kiislamu na kibinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: