Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa utaratibu wa kubeba washiriki wa hafla ya mabinti waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria awamu ya sita.
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Karbala, wameandaa hafla ya mabinti waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kupitia mradi wa (Maua ya Fatwimiyyah) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu).
Wanaosimamia ubebaji wa washiriki ni kitengo cha magari na utalii wa kidini chini ya Ataba tukufu.
Gari nyingi zenye ukubwa tofauti zimeandaliwa kwa ajili ya kubeba washiriki kutoka kwenye shule zao.
Wanafunzi wanaotarajiwa kubebwa ni (4500) kutoka kwenye shule (88), watapelekwa eneo la hafla na kurudishwa katika shule zao ndani ya siku mbili za hafla hiyo.
Atabatu Abbasiyya imeandaa vitu vyote vinavyo hitajika kufanikisha hafla hiyo.