Hafla ya kuwajibikiwa na sheria kwa wavulana wa shule za Al-Ameed imeshuhudia filamu inayo onyesha kuhusu kuwajibikiwa na sheria.

Hafla ya kuwajibikiwa na sheria wavulana wanaosoma katika shule za Al-Ameed awamu ya nne, imeshuhudia filamu fupi inayo onyesha kuhusu kuwajibikiwa na sheria.

Hafla imeandaliwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, chini ya kauli mbiu isemayo (Kuwajibikiwa kwangu na sheria nakuwa mwanaume wa mfano), inawashiriki (500).

Filamu imeonyesha program ya “Nusu ya Dini” na mtazamo wake pamoja na lengo la kufanywa hafla hiyo.

Aidha katika filamu hiyo kuna sehemu ya maswali na majibu kutoka kwa baadhi ya vinaja waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria wakiwa na walimu wao, pamoja na kuonyesha maandalizi yaliyofanywa kufanikisha hafla hiyo.

Hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria inalenga kujenga uwelewa wa kidini na kitamaduni, sambamba na kuandaa kizazi kinachoweza kubeba majukumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: