Wanafunzi wa shule za Al-Ameed wanaoshiriki kwenye hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria wanaelekea kwenye jukwaa la hafla.
Hafla imeandaliwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kwa ushiriki wa wanafunzi (500) waliofikisha umri wa miaka 15 kwa kalenda ya mwezi.
Wanafunzi (500) wanaelekea kwenye jukwaa kuu la hafla wakiwa katika upangilio mzuri huku wanasoma maneno yasemayo (Kufikisha kwangu umri wa kuwajibikiwa na sheria nakuwa mwanaume wa mfano).
Hafla imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wazazi waliohudhuria kwa wingi katika uwanja wa shule za Al-Ameed.
Hafla ya kuwajibikiwa na sheria kwa wavulana inalenga kuwajenga kidini na kitamaduni sambamba na kutengeneza kizazi ambacho kipo tayali kubeba majukumu.