Wanafunzi (4500) kutoka shule za Karbala wamesoma kiapo cha kuwajibikiwa na sheria katika uwanja wa majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla ya kuwajibikiwa na sheria imesimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa (Maua ya Fatuma) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zahara na ufuasi wa Zainabu) kwa ushiriki wa wanafunzi (4500) kutoka shule (88).
Mahfali imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na wazazi waliokuja kuangalia shughuli za hafla.
Kiapo walichosoma wanafunzi kina maneno yasemayo “Naahadi mbele ya shule yangu na wazazi wangu, kulinda heshima ya kuwajibikiwa na sheria, kufuata hukumu za Dini, tajitahidi kumtii Mola wangu, na kuwamfuata Mtume na Maimamu wangu, tawafanyia wema wazazi wangu, tatoa msaada katika mambo mema na ya uchamungu, tapambika na tabia njema, nategemea taufiqi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu”, ikafuatiwa na Duau-Faraj.
Asubuhi ya leo shughuli za hafla ya kuwajibikiwa na sheria zilianza kwenye uwanja wa majengo ya Abulfadhil Abbasi, zitakayodumu kwa siku mbili.