Siku ya pili ya hafla ya mabinti waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kutoka shule za mkoa wa Karbala, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amepiga picha ya Pamoja na mabinti hao.
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, zimefanya hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa mabinti wanaosoma shule za mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa (Maua ya Fatuma) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Fatuma na ufuasi wa Zainabu), kwa ushiriki wa wanafunzi (4500) kutoka shule (88).
Ratiba ya siku ya pili ya hafla hiyo imefanywa mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, viongozi mbalimbali wa kidini na kijamii na wazazi wa wanafunzi.
Ratiba ilikuwa na vipengele tofauti, ikiwa ni pamoja na kuonyesha filamu inayo elezea mradi, usomaji wa mashairi kutoka kwa Muhammad Yasiri na ugawaji wa zawadi kwa mabinti washiriki.