Atabatu Abbasiyya inatoa zawadi kwa waliochangia kufanikiwa hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa kisheria kwa wanafunzi wa kike.

Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa zawadi kwa waliochangia mafanikio ya hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa kisheria kwa mabinti wa shule za mkoa wa Karbala.

Utoaji wa zawadi ni sehemu ya muendelezo wa shughuli zinazofanywa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Karbala, kupitia mradi wa (Maua ya Fatuma) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu) na ushiriki wa wanafunzi (4500) kutoka shule (88).

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Aalu Dhiyaau-Dini, amekabidhi zawadi kwa watu waliochangia kufanikiwa hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria iliyofanywa katika majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria inalenga kujenga uwelewa wa mafundisho ya Dini kwa wanafunzi, ikiwemo kuwafundisha namna ya kutawadha, kuswali, kusoma surat Fat-ha kwa usahihi, kujenga mshikamano katika jamii sambamba na kujenga kizazi cha watu wanaoweza kubeba majukumu ya kiislamu na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: