Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na watumishi wa kitengo cha Habari ya kuripoti hafla ya maua ya Fatuma.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amepongeza kazi iliyofanywa na kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya ya kuripoti shughuli za hafla ya maua ya Fatuma.

Sayyid Dhiyaau-Dini amewaambia watumishi wa kitengo cha Habari kwenye hafla ya kuhitimisha shughuli za hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa wasichana wanaosoma katika shule za mkoa wa Karbala, hakika mmefanya kazi kubwa ya kuripoti shughuli zinazofanywa katika hafla hii na kubainisha malengo yake.

Muheshimiwa katibu mkuu amepongeza watumishi wa kitengo cha Habari na kusema kuwa wamesaidia kufikisha sauti ya Atabatu Abbasiyya katika picha yake halisi kwa waumini.

Mwisho wa maneno yake muheshimiwa katibu mkuu akatoa nasaha na muongozo kwa watumishi wa kitengo cha Habari, akawataka waendelee na kazi ya kufikisha picha na sauti ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wa walimwengu.

Hafla imefanywa kwa mara ya sita, chini ya usimamizi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu), kwa ushiriki wa wanafinzi (4500) kutoka shule (88).

Siku ya Jumanne katika uwanja wa majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zimehitimishwa shughuli za hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa mabinti wanaosoma katika shule za Karbala, kupitia mradi wa maua ya Fatuma zilizodumu kwa siku mbili.

Ratiba ilikuwa na vipengele vingi, iwemo kuonyeshwa filamu inayoelezea mradi wa kuwajibikiwa na sheria, usomaji wa mashairi kutoka kwa Muhammad Yaasiri na ugawaji wa zawadi kwa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: