Kitengo cha uboreshaji na manendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa warsha kuhusu mpango mkakati kwa viongozi wa idara za vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mkufunzi wa warsha hiyo Muhammad Hussein Jabaar amesema “Warsha hii inalenga uwezo wa viongozi wa idara na kubadilishana uzowefu katika kuweka mikakati ya kiutendaji kwenye idara zao”.
Akaongeza kuwa “Warsha imefanywa chini ya usimamizi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imekuwa na mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni uwelewa wa mikakati, uandaaji wa mikakati, tathmini ya ndani na nje, kupanga muda (time fram), namna ya kuandaa mpangilio wa muda, uwekaji wa vipaombele kulingana na mpango kazi”.
Warsha inafanywa ndani ya ukumbi wa idara ya uboreshaji na maendeleo endelevu, itadumu kwa muda wa siku (5) wanasoma saa (3) kila siku.