Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s).

Majlisi imeratibiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imejikita katika kueleza historia na utukufu wake, Majlisi imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) waliokuja kuomboleza na kukumbuka msimamo madhubuti wa Ammi yake Mtume (s.a.w.w).

Mawakibu za waombolezaji zimeenea kwenye Barabara za Karbala na sehemu ya Ataba mbili tukufu zikiomboleza msiba huo kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya.

Atabatu Abbasiyya imeweka utaratibu maalum wa kuomboleza msiba huo kila mwaka, ikiwa ni sehemu ya kuhuisha matukio yanayohusu watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: