Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amepokea ugeni kutoka taasisi ya (Ruhamaau-Bainahum) ya kijamii na watoto wanaolelewa na taasisi hiyo.
Kiongozi wa taasisi Sayyid Amiri Hassan amesema “Kikao chetu na Muheshimiwa Sayyid Swafi tumepata nafasi ya kuelezea taasisi yetu na utaratibu tunaotumia kulea watoto waliopo katika mazingira magumu kijamii, ambapo huwa tunawafanya wachanganyike na wenzao katika masomo”.
Akaongeza kuwa “Kusoma ni jambo kubwa kwa kila mtu duniani, na hupelekea kupatikana ukamilifu wa kila kitu, hupatikana madaktari wenye ubinaadamu na watu wanaofanya kazi kwa ufasaha kwenye sekta tofauti katika kutumikia taifa lao”.
Akaendelea kusema “Watoto wanaolelewa na taasisi wametoa shukrani zao kwa Sayyid Swafi kwani yeye ndio baba mlezi wa taasisi hii tangu ilipoanzishwa baada ya agizo la Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, pamoja na kueleza matarajio yao”.