Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Didah Mussawi, ametembelea ofisi za uboreshaji wa kiidara na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Muheshimiwa Mussawi katika ziara yake hiyo, ametoa muhadhara wa kutambulisha mkakati wa kuboresha utendaji wa kiidara, uliotokana na mtazamo wa Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, na umuhimu wa kujenga uwezo wa watumishi ili kupata ufanisi katika utendaji wao.
Katika muhadhara wake ameongea kuhusu baadhi ya mada zinazofundishwa katika shule za sekula na namna ya kufanyia kazi kwa vitendo mada hizo.
Akasema kuwa kusoma sekula kunafaida ya kielmu na kivitendo, unatakiwa kufanyia kazi elimu uliyonayo katika mambo ya kiidara.