Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha kongamano la Husseini awamu ya kumi na mbili kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Baghdad.
Atabatu Abbasiyya imeandaa kongamano kwa kushirikiana na kitivo cha Ibun Rushdi katika chuo kikuu cha Baghdad/ kitengo cha lugha ya kiarabu, chini ya kauli mbiu isemayo (Tukio la Twafu ni mnara wa mapinduzi katika mfumo wa kimaadili na msingi wa uadilifu kwa binaadamu).
Kongamano limepambwa na ujumbe kutoka kwa rais wa kitengo cha lugha ya kiarabu Dokta Hassan Baladawi, kisha vikaendelea vikao vya kongamano, ambapo jumla ya mada tatu za kielimu zimejadiliwa.
Mada ya kwanza ilikua inahusu misingi ya maadili kwa mwanaadamu katika tukio la Twafu kwa mtazamo wa kijamii, kisaikolojia na kihistoria, mada ya pili ikahusu athari ya lugha ya kiarabu katika tukio la Twafu, huku mada ya tatu ikijikita katika kueleza misingi ya islahi (kurekebisha) na athari yake katika mambo muhimu.
Mwisho wa kongamano yakasomwa maazimio yaliyoandaliwa na wanakongamano, kisha vikatolewa vyeti vya ushiriki.