Atabatu Abbasiyya imepiga kura maalum kwa ajili ya ibada ya Hija kwa watumishi wake.

Atabatu Abbasiyya chini ya katibu wake mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini imepiga kura maalum ya kuchagua watakao faulu Kwenda Hija miongoni mwa watumishi wa Ataba.

Kura hiyo imepigwa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), imehudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Katibu mkuu Sayyid Mustwafa Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Atabatu Abbasiyya imepiga kura maalum ya kuchagua watakaoenda Hija miongoni mwa watumishi wake, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, jambo hili hufanywa kila mwaka, mwaka huu Ataba imetenga nafasi (15)”.

Akaongeza kuwa “Majina yaliyofaulu kuingia katika kupigiwa kura yalikua (30)”.

Muheshimiwa katibu mkuu amesisitiza “Umuhimu wa Atabatu Abbasiyya kuongeza idadi ya wateule wa Kwenda Hija hata kwa kupitia sekta zingine, kutokana na wingi wa idadi ya watumishi wake na jinsi wanavyo fanya kazi kwa bidii ya kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: