Mradi wa Ajira bora unaendelea na ratiba ya kitamaduni kwa watumishi wa Ataba.

Mradi wa Ajira bora unaoendeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unaendelea na ratiba ya kitamaduni kwa watumishi wa Ataba katika ukanda wa kijani.

Mkufunzi wa mradi huo Sayyid Muhammad Yasiri amesema “Mradi unalenga kuhuisha turathi za Ahlulbait (a.s) na kuweka misingi ya kumkumbuka Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa namna sahihi na salama”.

Akaongeza kuwa mradi wa Ajira bora, umeanza utekelezaji wa ratiba yake kwa kutoa mihadhara ya kitamaduni kwa watumishi wa vitengo tofauti katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye eneo la ukanda wa kijani kusini ya mji wa Karbala”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ushiriki wa watumishi wake katika mradi wa Ajira bora inazingatia sana matumizi ya mitandao ya kijamii katika kufikisha ujumbe wa kimaadili, kidini na itikadi sahihi katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: