Balozi wa ufaransa amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma zake kwa mazuwaru.

Balozi wa ufaransa nchini Iraq Muheshimiwa Eriki Shofali amepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na huduma zake kwa mazuwaru.

Amepokewa na katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azhar.

Muheshimiwa Eriki Shufali amesikiliza maelezo kuhusu baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru na jamii.

Muheshimiwa Balozi amefurahishwa na miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ukiwemo mradi wa afya, kilimo, majengo na mingine mingi inayohudumia jamii.

Muheshimiwa Balozi amesema kuwa anapenda kutembelea Karbala kutokana na utukufu wa mji huo na ubinaabamu wa pekee unao onekana kwa raia wa Iraq.

Muheshimiwa Eriki Shufali na watu aliofuatana nao wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: