Kitengo cha habari na utamaduni kimefanya warsha kuhusu utaratibu wa faharasi katika chuo kikuu cha Basra.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya warsha mbili kuhusu utaratibu wa faharasi katika chuo kikuu cha Basra.

Mkuu wa kituo cha faharasi Sayyid Hasanaini Mussawi amesema “Katika wiki ya utamaduni na elimu inayo adhimishwa kwenye chuo kikuu cha Basra, kituo kimefanya warsha ya kuelezea faharasi ya kimtandao na faharasi saidizi”.

Akaongeza kuwa “Mihadhara imejikita katika kueleza kipimo cha (21) na kanuni za (RDA) na mhadhiri alikua ni Ustadh Ali Twalibu Kadhim”.

Warsha hiyo ni sehemu ya makubaliano baina ya kituo na vyuo vikuu vya Iraq, kwa lengo la kujenga uwezo wa mambo ya faharasi za kimtandao na karatasi kwa watumishi wa maktaba, kutokana na maelezo ya Mussawi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: