Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeanza ratiba ya usomaji wa Qur’ani kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ratiba hiyo inasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kila siku wasomi watatu hushiriki katika usomaji kwa kufuata ratiba maalum, usomaji huanza saa tisa jioni na hurushwa mubashara na mitandao ya kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel.
Miongoni mwa wasomaji wanaoshiriki ni Amaari Alhilliy, Qarari Almayahi na Thamir Fartusi.
Usomaji huo wa Qur’ani kila siku unaendana na utukufu wa kaburi takatifu, sambamba na kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani kila siku na kutoa nafasi ya kujifunza Qur’ani kwa mazuwaru.