Sayyid Swafi amesisitiza kuwa Ataba tukufu zinauwezo wa kuendeleza vipaji vya raia wa Iraq katika fani tofauti

Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, Ataba tukufu zinauwezo wa kuendeleza vipaji vya raia wa Iraq kwenye fani tofauti.

Ameyasema hayo alipokutana na mkuu wa Ataba na mazaru katika uongozi wa Wakfu-Shia Dokta Yaasir Alkatbi, na kusikiliza maelezo kuhusu shughuli zao na jinsi wanavyo shirikiana na Ataba tukufu pamoja na mazaru, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa mazuwaru.

Sayyid Swafi akasema kuwa “Hakika fikra iliyoanzishwa na Maimamu wa Ahlulbait (a.s) inapande mbili, kwanza upande wa kifikra, ambao wafuasi wao wanatakiwa kuelewa vizuri na kupambana na fikra potofu zinazochafua mafundisho ya uislamu sahihi uliofundishwa na Mtume mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s), upande mwingine ni wa kiroho, umesisitizwa na Maimamu (a.s) kuimarishwa kwa kutembelea malalo matakatifu na kufuata misingi ya kufanya ziara, pande hizo zinaumuhimu mkubwa sana kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Akasema kuwa, Atabatu Abbasiyya tukufu inaushirikiano mkubwa na marais wa Wakfu-Shia na Ataba zingine takatifu.

Akabainisha kuwa, Ataba tukufu ni taasisi huru, na zimelinda uhuru wake, jambo hilo limesaidia na kuziwezesha kutoa huduma tofauti kwa mazuwaru, zipo chini ya sheria maalum iitwayo, sheria ya idara za Ataba na mazaru za kishia namba 19 ya mwaka 2005, hivyo zinafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya Iraq na kwa kufuata kanuni maalum zilizowekwa.

Sayyid Swafi akasema kuwa, Ataba tukufu ikiwemo Atabatu Abbasiyya zinauwezo wa kuendeleza vipaji vya raia wa Iraq katika fani tofauti, zimekuwa imara kutokana na miradi zinazofanya inayosaitia kutangaza utamaduni wa Ahlulbait (a.s), na zinatakiwa kuwa na uwangalizi maalum kwa sababu zinagusa kundi kubwa la waumini.

Kiongozi wa Ataba na mazaru katika Wakfu-Shia Dokta Yaasir Alkatbi, amepongeza miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya ujenzi, utamaduni, elimu na nafasi yake katika kuhudumia jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: