Kuanza kwa hafla ya mwisho katika mradi wa Qur’ani kwenye vyuo vikuu vya Iraq.

Chuo kikuu cha Alkafeel suku ya Jumanne, kimeanza hafla ya mwisho ya mradi wa Qur’ani kwenye vyuo vikuu vya Iraq awamu ya nne katika mwaka wa masomo (2023 – 2024m).

Mradi umesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Mradi wa Qur’ani ulipambwa na vipengele vingi yakiwemo mashindano ya usomaji wa Qur’ani, mashindano ya kuchagua andiko bora la wahitimu, mashindano ya kusoma Qur’ani kwa kuangalia na kwa kuhifadhi, usomaji wa Qur’ani kwa njia ya mtandao, safari za kidini, maonyesho ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Kufa na Qadisiyya.

Mradi umejikita katika kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani na kufuata mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwa wanafunzi, sambamba na kuwalinda na fikra potofu zinazoingizwa kwenye jamii na kuwapa nafasi ya kukuza uwelewa wao kuhusu Qur’ani na utamaduni wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: